Maneno ya Manara kwa Rostam 'Ukiingia Yanga unaanza kulipa madeni kama yote'



Baada ya Rostam Aziz kusema yeye ni shabiki wa timu ya mpira ya Yanga alipoulizwa na Rais na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.  Hatimaye Msemaji wa timu ya Simba,  Haji Manara amemuomba Rostam kuisaidia timu ya Yanga.

Manara kupitia ukarasa wake wa Instagram amesema kuwa Yanga walivyo na njaa akiingia ataanza kulipa madeni kama yote na mishahara.

"Sasa Shekh Rostam kwa kuwa umedeclere leo mbele ya bwana mkubwa kuwa ww ni Yanga na hali zao ni taabani sana kiasi cha kumlilia mtu aendelee kuwaongoza!! Hebu njoo huku kwenye mpira basi, au ww Yanga jina tu," aliandika Manara.

Aliongeza "Na walivyo na njaa ukiingia tu unaanza kulipa madeni kama yote na mishahara!!
Nategemea povu la kufa mtu toka Mbuteni."