Kiungo mshambuliaji, Samir Nasri ambaye sasa yuko huru baada ya kusitisha mkataba wake na Anatalyaspor ya Uturuki, anafanya vipimo vya afya kujiunga na klabu ya West Ham United ya nchini Uingereza.
Mshambuliaji huyo kwa sasa anatumikia adhabu baada ya kusimamishwa kwa miezi 18 kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kupambana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Ripoti mbalimbali nchini Uingereza, zinadai kuwa mchezaji huyo atafanya vipimo vya afya kwenye klabu hiyo ya mjini London.
Nasri ambaye kwasasa ana miaka 31 atakuwa akikunja mfukoni kiasi cha £ 80,000 kwa wiki kama atasaini mkataba katika klabu hiyo.
Nasri, endapo atakamilisha dili la kujiunga na West Ham atakuwa ameungana na kocha, Manuel Pellegrini, ambaye alimfundisha miaka mitano iliyopita katika klabu ya Manchester City.