Rais Magufuli: Ninyi Mawaziri mlioteuliwa msidhani mtapendwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaambia Mawziri aliowateua wasidhani kama watapendwa na baadhi ya Wabunge.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 12, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua Jumamosi wiki iliyopita.

"Ninyi Mawaziri mlioteuliwa msidhani kama mtapendwa na baadhi ya Wabunge kwasababu wapo baadhi ya Wabunge wachache sijui nao ni watano wangapi wao kila siku wanawazaga Ubunge tu na Uwaziri na mimi nimeshawasahau, utakuta wanatukana kila kitu wanafikiri they no more (wanajua sana) Kazi hizi ni ngumu ndugu zangu ni kujisucrifies sasa i hope nimezungumza ya jumla," alisema Rais Magufuli.

"Lakini niwashukuru sana Mh. Tizeba na Mwijage ninyi ni wazalendo mmeonyesha ushujaa wa pekee mmekuja kwasababu mmejua hizi kazi ni temporary kwasababu hata maisha yenyewe ni temporary," aliongeza.
Mpya zaidi Nzee zaidi