Nedy Music afunguka kuhusu kufanya kolabo na Yvonne Chakachaka


Msanii wa muziki Bongo, Nedy Music amejibu iwapo alikutana na Yvonne Chakachaka walipanga kufanya wimbo wowote.

"Sisi tunasema tupo bize lakini mama naye yupo bize sana, ni mtu ana ratiba za kutosha na tumekutana mara mbili tumezungumza lakini hatukupa ule muda mzuri wa mimi kuweza kuyazungumza mengi," amesema Nedy Nedy kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM.

Nedy Music na Yvonne Chakachaka walikutana nchini Ghana wiki iliyopita kwenye utoaji wa tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA).





Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items