Neno la DC Jokate kwa Rais Magufuli baada ya uteuzi



Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,  Jokate Mwegelo amempongeza Mkurugenzi Mkuu mteule wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine Sayi ambapo amemtaka awawawakilishe vijana vizuri.

 DC Jokate pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaamini vijana wenye sifa na weledi kufanya vitu vikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.

Jokate ametoa ujumbe huo leo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, ambapo ameandika  kuwa ana ufahamu uwezo wa Japhet na kuamini kuwa suala la Korosho atalisimamia vyema.

"Rais kaomba leo Ikulu uthibitishwe kijana mdogo uwe Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania. - TADB. Tunaamini kwa akili na uwezo wako mkubwa sasa wakulima watafutwa machozi yao na hili la korosho utalisimamia vyema. Sina shaka na uwezo wako kabisa. Mwenyezi Mungu aendelee kukuongoza . Asante Mhe Rais kwa kuendelea kuamini vijana wenye sifa na weledi kufanya vitu vikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu," ameandika Jokate kupitia ukurasa wake wa Instagram leo.

Japhet Justine Sayi alikuwa kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo kabla ya leo Rais Magufuli kuelelekeza Waziri husika anayeshughulikia benki hiyo kumthibitisha Rasmi kuwa Mkurugenzi mkuu.


Mpya zaidi Nzee zaidi