Watu 40 wafariki katika ajali ya treni

Watu 40 waripotiwa kufariki katika jali ya treni ya mizigo iliotokea katika jimbo la Lwango  karibu na  eneo la Samba Mashariki mwa Congo.

  Kulingana na taarifa zilizotolewa na  vyombo vya habari vy Congo katika eneo la tukio, terni hiyo iliondoka katika reli na kusababisha ajali hiyo iliyopelekea maafa .

Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikielekea mjini Lubumbashi Kusini mwa Congo.

Watu 40 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa.

Shirika la reli la Congo limefahamisha kuwa huenda mwendo kasi ndio sababu ya ajali hiyo na kufahamisha kuwa uchunguzi umeanzishwa kubaini sababu ya ajali hiyo.

Ajali za treni nchini humo hutokea mara kwa mara  kutokana na  uhaba wa miundombinu.

Mpya zaidi Nzee zaidi