RC Mwanri ahaidi matrekta mia


Na Rahel Nyabali, Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri  ameahidi matrekta mia moja kwa lengo la kuboresha kilimo mkoani Tabora

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wajasiliamali Wilaya ya Tabora mkoani Tabora lengo ikiwa kuimalisha sekta ya kilimo.

"Tabora tuamke uwe mfano wa kuigwa kila mmoja lazima alime kulimo cha kisasa iwe mhogo, pilipili, Tikitimaji, mazao yote yanatakiwa yapandwa kwa masitari ili tuzalishe na ziada" amesema Mwanri.

Hatahivyo amewataka wananchi mkoani humo kuishi kwa hofu ya mungu ili kuweza kufanikiwa katia mambo yao nakuachana mira potofu.

Kwa upande mwingine katika jukwaa la wajisiliamali lilofanyika katika ukumbi wa AMCTA wilayani Tabora Mkoa wa Tabora lengo likiwa ni kupanua fursa za uwekezaji kwa wajasilimali mkoani humo.

Amesema kuwa wanataka Tabora iwe kitovu cha uwekezaji kwani vongozi wakubwa na maprofesa walianzia mkoani hapa kilichobaki ni kushikamana na kujikwamua.

Aidha Mwanri amesema licha ya mkoa huo kuwa na historia kubwa katika Taifa la Tanzania lakini bado wako nyuma kinaendeleo jambo ambalo linawakosesha raha wakazi mkoani humo.