Tazama matukio katika picha kutoka Bungeni leo – Novemba 12, 2018

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu swali kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha sekta ya michezo nchini wakati wa kikao cha tano Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Jijini Dodoma, Ambapo kikao cha tano Mkutano wa 13 kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge. Kipindi cha Maswali na Majibu kiliendelea na wabunge walihoji maswali na kujibiwa na Serikali: 

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha tano cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifafanua jambo wakati akijibu swali la Mhe. Asha Jecha(hayupo pichani) kuhusu ukatili wa watoto katika kikao cha tano cha Mkutano wa 13 wa Bunge jijini Dodoma leo
Mbunge wa Hanang’i Mhe. Mary Nagu akichangia hoja kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2019/2020 katika kikao cha tano Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma