Usalama SC yaendelea kupoteza, yapanga kuwatema wengi dirisha dogo

Na John Walter-Babati

Timu ya mpira wa Miguu Usalama Sc kutoka Mkoani Manyara inayoshiriki ligi daraja la pili  imeendelea kufanya  vibaya mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi daraja la pili Tanzania Bara [SDL] baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kitayosa Fc ya Kilimanajaro  katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Singe Sekondari mjini Babati .

Matokeo hayo yanawapa wakati mgumu Usalama kuingia katika kusaka tiketi ya kupenya ligi daraja la kwanza kwani imeshapoteza mchezo wa nne Mfululizo,miwili wakiwa nyumbani.

Mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute ulikuwa wa kuvutia katika muda wa kipindi cha kwanza kabla ya kipindi cha pili mchezaji wa Kitayosa  Fc kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga ngumi mmchezaji wa Usalama Sc.

Matokeo hayo ya sare  yanaifanya Usalama Sc ifikishe pointi moja huku wenzao Kitayosa Fc wakifikisha pointi mbili katika michezo minne.

Ratiba inaonyesha imebakiza michezo tisa kuendelea kutetea nafasi ya kuingia ligi daraja la kwanza huku vugu vugu la wachezaji kutemwa kwenye dirisha dogo la usajili likitanda Usalama sc.

Taarifa ambazo Muungwana Blog inazo ni kwamba Uongozi wa timu ya Usalama Sc uliketi na kuzungumza na wachezaji na kulipa madeni yote ya wachezaji.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa timu hiyo ambaye hajapaenda jina lake litajwe alisema wameamua kuwalipa  wachezaji wote  pesa zao zote ili watakaoachwa waondoke pasipo malalamiko  ili mtu anapoondoka anyanyue mabegi yake bila kugeuka nyuma.
Mpya zaidi Nzee zaidi