VETA yaipa mchongo Takukuru kuhusu malipo yafidia ya eneo la ardhi


Na.Ahmad Mmow,Lindi.

Chuo cha ufundi stadi (VETA) Mkoa wa Lindi kimeomba mamlaka  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuingilia kati sitofahamu ya malipo yafidia ya eneo la ardhi yaliyofanywa na chuo hicho.

Ombi hilo lilitolewa na mkuu wa chuo hicho,Samuel Nng'andu wakati wa mahafali ya tano ya wahitimu wa mwaka huu wa 2018.Yaliyofanyika chuoni hapo katika manispaa ya Lindi.

Nng'andu ambaye  aliwatangazia wazazi,walimu nawanafunzi waliokuwepo kwenye mahafali hayo kwamba atastahafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria mwaka huu.Allisema kinaeneo kwa ajili ya ujenzi na tayari kilishalipia fedha ambazo zilitumika kuwalipa wanachi waliochia maeneo yao.

Alisema eneo hilo ambalo linatarajiwa kutumika kwa ujenzi wa chuo kwa huduma za hosteli na mafunzo lenye ukubwa wa mita za mraba 45,299.00 tayari limelipiwa na VETA kwa awamu nne.Ambapo shilingi 145,720,500.00 zimelipwa.

Hata hivyo mkuu huyo wachuo alisema pamoja na kutekeleza masharti yaliyopo kwa mujibu wa sheria,lani kumeibuka mgogoro unaosababisha kuibuka mashaka kwamba shilingi hizo 145.72 milioni hazikuwafikia na kuwanufaisha walengwa ambao walipaswa kulipwa.

Alisema hofu inasababishwa madai mapya yaliyopelekwa wakati wao walitimiza masharti.Hata hivyo umeibuka mgogoro mpya kutoka kwa mwananchi anayetaka eneo lake lifanyiwe uthamini upya.Hali inayosababisha VETA kidaiwe malipo mengine yenye jumla ya shilingi 24,813,410.59.

"Kwetu sisi inatia shaka natungeomba ikiwezekana uhakiki wa malipo ya shilingi 145.72,ufanyike upya ili kuthibitisha kama walionufaika ndio walengwa.Hiyo itaondoa mashaka ya madai hayo mapya,"alisisitiza Nng'andu.

Alimuomba katibu tawala wa mkoa wa Lindi,Rehema Madenge aliyekuwa mgeni rasmi katika mhafali hayo kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa Lindi nakwa niaba ya serikali.Changamoto hizo zitatuliwe ili kuongeza kiwango cha udahili ili jamii ya Lindi na taifa kwa jumla iweze kunufaika na uwepo wa chuo hicho kupitia mafunzo waliyopata wanafunzi wake.

Aidha Nn'gandu alitoa wito kwa serikali ya mkoa kutumia weledi na uzoefu wake iwahamasishe wananchi wa mkoa huu wa Lindi wawapeleke vijana wao wakajiunge na chuo hicho.Kwani bado kina uwezo mkubwa wakupokea wanafunzi kuliko idadi ya wanafunzi waliopokewa na waliopo.

Alisema chuo hicho kimeendelea kufanya udahili wa wanafunzi kila mwaka hadi kufikia idadi ya wanafunzi 360 mwaka huu.Ambapo idadi ya waschana waodahiliwa imeongezeka kutoka 29 ya mwaka 2012 mwaka ambao chuo kilianza kutoa mafunzo,nakufikia wanafunzi 124.Idadi ambayo hairidhishi,hivyo juhudi za makusudi kutoka kwa wadau zinahitajika.

"Katika kipindi cha mafunzo mwaka huu tulipewa nafasi ya kudahili wanafunzi 506.Hata hivyo tumedahili 360 ikiwa ni upungufu wa wanafunzi 146 ambao sawa na asilimia 29,"alisema Nng'andu.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Lindi,Rukia Madenge aliuagiza uongozi wa chuo hicho uhakikishe unaongeza idadi ya wanafunzi na ubora wa mafunzo ili ajira zisichukuliwe na wageni.Lakini pia mafunzo yanayotolewa yakidhi mahitaji ya soko la ajira katika  sekta rasmi na isiyo rasmi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Madenge alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kuchangamkia fursa zinazotokana na chuo hicho kwa kuwapeleka vijana wao wakapate mafunzo.Akiwaonya kwamba wasipotumia fursa hiyo watabaki kuwa watazamajj na wasindikizaji pindi ajira zitakapochukuliwa na wageni ambao watatoka nje ya mikoa ya Lindi na Mtwara.

Chuo cha ufundi stadi cha Lindi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 hadi mwaka huu kimedahili wanafunzi 1519(wavulana 1091 na waschana 428.Ambapo kimetoa wahitimu 631,kati yao wavulana 451 na waschana 180.Huku kikiwa kimezalisha ajira 250 kupitia wahitimu wa  mafunzo mbambali waliyopata kwenye chuo hicho.