Wafungwa 113 watoroka gerezani

Wafungwa 113 wametoroka gerezani katika jimbo la Aceh nchini Indonesia.

Kwa mujiu wa taarifa zilizotolewa na gazeti la Kompas,Katika  gereza lililopo  Banda Aceh lililokuwa na wafungwa 726 kulitokea vurugu jana jioni na hatima yake wafungwa 113 walitoroka.

Baada ya tukio hilo wafungwa 20 miongoni mwa waliotoroka walikamatwa maeneo mbalimbali na kurudishwa gerezani. Msako bado unaendelea kutafuta waliosalia.

Mpaka sasa iliyopelekea vurugu hizo hazijajulikana, uchunnguzi kuhusiana na tukio hilo umeanza kufanywa.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items