RC Gambo aelezea ziara ya Rais Magufuli Arusha



Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,ametoa Taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusiana na ziara ya Mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ambapo ameeleza kuwa Rais katika ziara hiyo kesho atazindua kituo cha forodha na baadae atazungumza na wananchi waishio mji huo wa Namanga na wilaya ya Longido.

Kituo hicho kimejengwa na nchi za jumuia ya afrika mashariki kwa ajili ya kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji pia kuondoa vikwazo na usumbufu waliokuwa wakipata wananchi kutoka nchi moja kwenda nyingine hivyo kujengwa kwa kituo hicho ni kurahisisha huduma hiyo.

Katika tukio lingine jeshi la polisi limekabidhi mbwa wawili kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na uvushaji wa bidhaa kwa njia ya magendo .Gambo,amesema kuwa mbwa hao wamekabidhiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro, jana ambapo mbwa hao watatumika kulinda mpaka huo wa Namanga,wilayani Longido ambao upo kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania ,

Gambo,amesema kuwa Rais Magufuli, Desemba 2 siku ya Jumapili rais ataweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha,AUWSA.

Amesema kuwa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 520 ukikamilika utakuwa umemaliza tatizo la upungufu wa maji katika jiji la Arusha na maeneo ya jirani ya wilaya ya Arumeru ambako ndiko kwenye chanzo kikuu cha maji yanayosambazwa jijini Arusha.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items