Wahitimu waaswa kutafuta fursa badala ya kusubiri fursa ziwafuate


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,  Jakaya Kikwete leo amewatunuku wahitimu 4742 wa shahada za uzamivu, uzamili, shahada za awali, stashahada na astashahada mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Mahafali hayo ya 48 ya kuwatunuku wahitimu hao yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza katika mahafali hayo Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Willium Anangisye amewaasa wahitimu hao kutafuta fursa badala ya kusubiri fursa ziwafuate.

Muwe na hulka ya kuthubutu mambo ambayo yanaonekana magumu, hata pale mnaposhindwa kufikia mafanikio mliyotarajia, msife moyo, endeleeni kuwa na ari ya kujaribu tena," aliongeza.

Kati ya wahitimu hao 4742, waliotunukiwa shahada za uzamivu ni 74, huku 435 wakitunukiwa za umahiri, 15 za umahiri wa uzamili na 4,137 wakitunukiwa shahada za awali.