Hayo yamesema leo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Dakarro wakati wa kukabidhi vitanda viwili vyenye thamani ya Milioni 2.9 kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto leo jijini Arusha vilivyotolewa na wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kwa kituo cha Afya Kaloleni jijini Arusha kama ishara ya upendo kwa wagonjwa katika Kongamono la Wataaluma wa Maendeleo ya Jamii Nchini.
Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii pia wameshiriki kufanya usafi katika kusaidia ujenzi katika Kituo cha Afya Jijini Arusha kuashiria kuanza kwa kongamano la siku tano la wanataaluma wa fani ya maendeleo ya Jamii hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha pia alitoa wito kwa wataalamu hao kwenda mbali zaidi ya kuhamasisha vikundi vya vijana, akina mama na walemavu bali wafanye uchechemuzi kwa jamii kushiriki katika hatua za kujiletea maendeleo kwa kutumia rasilimali walizonazo.
Aidha Bw. Dakarro alitaka wataalamu hao kuhamasisha jamii kuzingatia usafi katika mazingira yao ili waweze kuondokana na magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu na magonjwa ya kuhala lakini kufanya mazoezi suala ambalo litaepusha jamii kupata magonjwa na hivyo kuokoa fedha nyingi za serikali.
“Kuhamasisha Jamii kufanya mazoezi na usafi kutafanya watu wengi kuepuka magonjwa ya kisukari na presha na kwa kufanya hivyo wagonjwa wanaofuata dawa za magonjwa hayo hapa hospitalini watapungua na kuokoa fedha nyingi za Serikali. aliongeza Bw. Dakarro.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema kuwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii ni chachu ya Taifa kufikia uchumi wakati na kwa kushiriki kazi za kuhamasisha Jamii kujiletea maendeleo wanaokoa fedha nyingi ambazo zinatumika katika shughuli nyingine za Serikali.
Aidha Bw. Golwike Sera ya Maendeleo ya Jamii ya Mwaka 1996 inahamasisha Jamii kujiletea Maendeleo kutegemea rasilimali zilizopo na kutaja kitendo cha wanataaluma wa fani hiyo kushiriki ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Kaloleni jijini Arusha kuwa unaweza usione mchango wao kwa wakati huo lakini kimeokoa fedha nyingi za serikali.
‘’Kwa kila kazi tunayofanya uwa tunaokoa fedha nyingi kazi yetu ni kuhamasisha jamii kujiletea maendeleo kwa kutumia fedha na rasilimali zilizopo hivyo kuchechemua ukuaji na ustawi wa Jamii Nchini. ‘’Aliongeza Bw. Golwike.
Aidha Bw. Golwike aliongeza kuwa yeye na wataaluma ya Maendeleo ya Jamii wanaamini jamii inyaoumwa haiwezi kushiriki katika kazi maendeleo ndio maana wataalamu hao wameamua kushiriki kusaidia ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya kwa lengo la kusaidia Jamii kuwa na Afya bora kushiriki katika ujenzi wa Tanzania kuelekea uchumi wa kati.
Aidha rais wa muda wa chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) Bw. Wambura Sunday amesema kuwa watahakikisha anafanikisha azma ya wataalum wa Maendeleo ya Jamii kuanzisha chama cha kitaaluma na kutaka hiyo na kuwasihi wataalam hao kuwa na umoja na mshikamano.
Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wanakutana kwa siku tano mjini Arusha kushiriki kongamano la mwaka la wataalam wa maendeleo ya Jamii kwa lengo la kubadilishana uzoefu na mbinu za utekelezaji wa Sera za Maendeleo ya Jamii ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi na umahili.
