11/08/2018

Waziri wa sheria wa Marekani ajiuzulu

Waziri wa sheria wa Marekani Jeff Session amejiuzulu wadhifa wake.

Katika barua yake  ya kujiuzulu aliandika " Nawakilisha barua yangu ya kujiuzulu kama ulivyotaka, nikushukuru kwa fursa hii uliyonipa" alisema Jeff.

Jeff alisema kwa muda wote aliofanya kazi katika wizara hiyo alifanya kazi kwa morali kubwa, aliishukuru pia timu yote ilyokuwa ikifanya kazi chini yake.

Kuhusiana na mada hii rais Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter " Tunakushsukuru waziri wa sheria  Jeff Session kwa kazi yako na kwa nia njema tunakutakia kila kheri"

Trump amemtangaza kiongozi wa wafanyakazi wa wizara hiyo ya sheria, Matthew G. Whitaker,kushikilia nafasi hiyo ya waziri wa sheria kwa muda.