Yanga watoa kauli hii juu ya BMT


Katibu Mkuu wa Matawi ya Yanga, Boaz Kupilika ameibuka na kueleza kuwa hawapo tayari kusimamiwa uchaguzi wao mkuu na Kamati ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Hatua imekuja mara baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kupitia Katibu wake, Alex Mkenyenga kuitaka TFF isimamie uchaguzi huo ambao unatakiwa kukamilika ndani ya mwezi mmoja.

Kupilika amepinga kwa msisitizo maamuzi hayo akieleza wao kama Yanga wana maamuzi ya kufanya vitu kwa kujisimamia na si kuongoza na mtu mwingine yeyote.

Katibu huyo amehoji kwanini wameambiwa wao pekee huku akiwataja Simba kuwa nao kamati yao ya uchaguzi ina mapungufu lakini hawajapewa onyo lolote.

"Hatuwezi kusimamiwa na TFF kufanya uchaguzi wetu, sisi tunajiongoza wenyewe na si kwa kushinikizwa na mtu mwingine yeyote. Mbona Simba wao pia kamati yao ina mapungufu lakini hawajaambiwa chochote kile?" alisema.

Mkeyenge alisema Yanga haina kamati ambayo inajitsheleza hivyo ni vema TFF wakausimamia na mwisho wa siku kumpata kiongozi ambaye amestahili.