Beki mpya wa Simba akutwa na makubwa


Beki mpya wa Simba,  Zana Coulibaly ambaye ni raia wa Burkina Faso, amewekwa kando kwa muda ili kupewa muda wa kuzoea mazingira ya timu.

Beki huyo ambaye amesajiliwa hivi karibuni akitokea klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast ni mbadala wa Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa beki huyo kwa sasa hayupo kwenye mipango yake hivyo hana muda wa kuhangaika naye.

"Zana yupo hapa anafanya mazoezi na wenzake ila sihangaiki naye sana kwa kuwa hayupo kwenye mpango  katika mchezo wetu dhidi ya Nkana FC, hivyo nimemuacha na wenzake ili aweze kuzoeana nao na usajili wake ukikamilika tutakuwa naye katika kazi," alisema.