.

12/06/2018

Hapa ndipo zilipoishia kolabo za Linah na RachaelMsanii wa Bongo Fleva, Linah ameeleza sababu ya kutoendelea kutoa ngoma pamoja na Rachael baada ya kuahidi kufanya hivyo.

Muimbaji huyo kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM ameeleza kuwa walipanga baada ya kuachia wimbo, Same Boy kuendelea kutoa nyimbo zao hata hivyo Rachael amekuwa mtu mwenye shughuli nyingi nje ya muziki,

Kutokana na hilo ndipo Linah akaendelea kutoa nyimbo zake binafsi ambapo hadi sasa ametoa nyimbo kama Koleza na Tuliza Boli.