F Jinsi ya kupata wazo bora la biashara | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Jinsi ya kupata wazo bora la biashara

Kisaikolojla kila mtu ana mawazo bila kujali ni mazuri au mabaya. Wakati mwingine binadamu huwa na mawazo mazuri ambayo kama atayaendeleza na kuyafanyia kazi yanaweza kubadili kabisa maisha yake.

Mawazo humfanya mtu awe alivyo, aonekane vile anavyoonekana. Mwenye akili, mpole, mkorofi,mwema au mkatili. Haya yote ni matokeo ya mawazo aliyonayo mtu kichwani mwake.

Kila siku tunasikia watu wanasema nina pesa ila sijajua nifanye biashara au mradi gani. Wakati mwingine utasikia mtu akisema nina wazo zuri la kufungua biashara au mradi tatizo langu mtaji sina.

Katika kuwaza kwao watu hawa mwisho hujikuta muda umeenda, umri umesonga bila hata kutekeleza wazo moja alilopanga. Mwenye pesa amekaa na pesa hadi imekwisha kwa kutatua matatizo ya aina mbalimbali.

Soma; Njia Tano (5) Bora Za Kukuza Biashara Yako.

Mwenye wazo kawaza mpaka kawa ua mtaji hana na wazb limechina mwisho anakata tamaa na kuamua kufanya kazi asiyotaraji kuifanya ili kujikimu na mahitaji ya kila Siku katika maisha.

Ni Kitu gani kifanyike ili watu hawa waweze kufanikiwa? Mwenye wazo na mwenye pesa? usiumize kichwa Kisuda nitakupa slri yake leo. Kabla sijaeleza namna gani ufanye nikudokezee siri moja muhimu katika mafanikio.

Ili mtu yeyote iwe mimi au wewe uweze kufanikiwa unahitaji vitu vinne.

1. MAARIFA/UJUZI juu ya jambo unalotaka kufanya.

2. WAZO BORA NA ZURI la kukuongoza hatua kwa hatua lenye taarifa sahihi juu ya mradl au biashara husika.

3. WATU WAZURI wa kushlriklana nao. Hakuna kazl au mradi unaoweza kuufanya peke yako Ila kushlriklana na watu. Hlvyo nl Iazlma upate watu maklnl na sahlhl wa kushirikiana nao.

4. MTAJI /PESA ya kuanzishia mradi lakinl zlngatia kuwa pesa sl chochote katika mradi au biashara hata uwe na mamilioni ya shilihgi kama huna hlvyo Vitu vlnglne wazo,maarifa na watu sahihi sahau kuhusu MAFANIKIO utaangukia pua tu. Kisaikolojia pesa haileti mawazo, baIi mawazo ndiyo huleta PESA. Na hii ndio Imani yangu na falsafa yangu Kisuda katika maisha yangu ya mafanikio.

Soma; Mambo Ya Kuzingatia Katika Biashara.

Sasa nitoe njia 5 za kuweza kukusaidia wewe rafiki yangu katika kupata wazo la biashara ili uweze kufanikiwa kirahisi kwa wewe mwenye pesa na mwenye wazo:

1.Tafuta _uhitaji wa watu/ tatizo Iinalowasibu watu kisha tafuta namna ya kuwatatulia shida /tatizo lao utapata pesa nyingi sana.

2. Boresha wazo la mwingine'. Hapa («kuangalia tu mapungufu ya mtu katika kazi au biashara halafu una boresha utendaji kazi na utaona mabadiliko makubwa katika kazi au biadhara yako. Kamwe usiige wafanyavyo wengine utapata matokeo

yaleyale wapatao wao badili njia.

3. Hamlsha wazo kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hapa na maanlsha uklona mradi au biashara sehemu sl lazima nawe ukafanyie pale unaweza anzisha wazo kama hilo sehemu tofauti na ukafanikiwa sana.

4. Rahisisha mchakato au upatikanaji wa huduma au bidhaa fulani badala ya watu kuifuata sokoni au mjini wapelekee wewe nyumbani kwao watakulipa “pesa nyingi na gharama ya usaliri kwa nini wakulipe? Umewaokolea muda wao ili wafanye mambo mengine na pia wamepata wanachotaka kwa wakati.

5. Tengeneza uhitaji kwa watu. Hapa ni kubuni Kitu cha ziada ambacho watu wanakihitaji Iakini kutokana na muda au umbali wanaona kama hakina umuhimu sana kwao. Mfano simu za mkononi zimekuja baada ya barua kuonekana kuchelewa kuwaflkia wahusika leo hii taarifa ya dakika 10 imeshasambaa nchi nzima.

Haya sisi wataalamu tunaita ni kutengeneza mahitaji ya ziada kwa watu ili wakulipe pesa. UWEZO WAKO WA KUJA NA MBINU AU WAZO JIPYA TOFAUTI NA MAZOEA YA WATU NDIO.CHANZO CHA MAFANIKIO YAKO.