MKAZI wa mtaa wa Nyasubi, Kahama mkoani Shinyanga, Monalisa Maduhu (42), anayefanya kazi ya mama lishe, anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga.
Tukio hilo lilitokea juzi majira ya 10.00 jioni katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama, baada ya mtuhumiwa kufika hospitalini hapo na kumkuta mama wa mtoto huyo Elizabeth Yohana (21) akiwa ameshajifungua.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule, alisema mtuhumiwa huyo alimwomba mama wa mtoto huyo amsaidie kumbeba na kumtuma akanunue maji ya kunywa ndipo akatoroka naye.
Alisema baada ya mtuhumiwa huyo kuondoka na mtoto huyo mchanga aitwaye Angel Hamisi, mama yake mzazi kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali, walitoa taarifa polisi na uchunguzi ukaanza mara moja.
Alisema polisi kwa kushirikiana na wauguzi wa hospitali hiyo pamoja na mama mzazi wa mtoto, walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake akiwa na mtoto huyo.
“Baada ya kumkamata mtuhumiwa na kumhoji, alikiri kumuiba mtoto huyo mchanga kwa madai kuwa anataka kuongeza idadi ya kuwa na watoto wawili wa kike kwa kuwa anaye mmoja tu na wa kiume mmoja,” alisema Haule.
“Mtoto huyo mchanga tumeshamkabidhi mama yake mzazi na sasa bado wapo katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi ya kuimarisha afya yake kwani tangu aibwe ana siku mbili hakupata huduma ya mama ili kupata kinga mbalimbali za kiafya,” aliongeza.
Aidha alisema jeshi bado linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi na kwamba hivi karibuni atafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yanayomkabili kwa mujibu wa sheria.