.

12/06/2018

Matola atuma salamu hizi Simba

Kocha wa timu ya Lipuli, Seleman Matola ambaye aliwahi kuichezea klabu ya Simba na kua nahodha wa klabu hiyo amewatumia salamu za pongezi wachezaji wa Simba na kuwataka wasibweteke na matokeo waliyopata kwa kuwa wana kazi nzito kuhakikisha wanapenya hatua zote.

Matola amesema kuwa wakati wa Simba kuweza kupenya kimataifa ni sasa wanapaswa kujituma zaidi kusonga mbele kwa kuwa kazi ndo kwanza inaanza.

" kwa hapo walipofikia si hatiua mbaya wanapswa pongezi ila wasijisahau kuendelea kupambana wana safari ndefu kutafuta mafanikio, hapo walipofikia safari ndo inaanza kupeperusha bendera ya taifa," alisema.

Simba wamefanikiwa kupenya hatua ya awali kwa ushindi wa nje ndani mbele ya Mbabane Swallows ya Eswatini kwa ushindi wa mabao 8-1, mchezo wao unaofuata hatua ya kwanza ni dhidi ya Nkana FC.