Mtandao wa Facebook wapigwa faini

Bodi ya Ushindani ya Italia (AGCM) imeulipisha mtandao wa Facebook faini ya  kiasi cha  euro milioni 10.

Katika taarifa iliyoandikwa na Bodi ya Ushindani ya Italia, ilielezwa kuwa watumiaji wamelipishwa euro milioni 10 kwa kutumia taarifa zao za kibinafsi kwa madhumuni ya biashara kinyume na sheria katika mtandao wa Facebook.

Kwa mujibu wa habari,hatua hiyo imeenda kinyume na sheria kifungu namba 21 na 22 cha matumizi ya Facebook na kwamba watumiaji walifanya biashara bila ya kutoa taarifa.

Pia ilibainisha kuwa Bodi ya Ushindani ilmegundua kuwa hakuna mfumo wa kutoa onyo moja kwa moja wakati tovuti inaposhambuliwa.