Yanga yaja na kauli hii kuhusiana na Kakolanya


Wakati kipa namba moja wa Yanga, Beno Kakolanya akiwa amegoma kuendelea kuitumikia timu yake, uongozi wa klabu hiyo umesema mpaka sasa haujui Kakolanya wapi alipo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema kuwa wao hawawezi kumfuatilia mchezaji ambaye hayupo kambini.

Nyika amefunguka kueleza kwamba Kakolanya bado ni mchezaji wa Yanga lakini jukumu la kuanza kumfuatilia wapi alipo si lao.

Aidha, amesema wanasubiria mpaka atakaporejea kambini ndipo watajua kipi kinachomsumbua huku akieleza hakuna anachowadai kwa sasa.

Wakati Nyika akifunguka hayo, inaelezwa kuwa Yanga imeshaanza mazungumzo na kipa mwingine kutoka nje ya Tanzania kuja kuchukua nafasi yake.