Aliyewahi kugombea Ubunge Tarime apiga tafu ujenzi wa madarasa



Na. Clonel Mwegendao

Aliyewahi kuwa Mgombea Ubunge wilayani Tarime katika Jimbo la Tarime Mjini mkoani mara Michael Kembaki amezidi kutekeleza ahadi zake ambapo hii leo ametoa mabati 50 aliyokuwa amehaidi 2015 wakati wa kampeini za uchaguzi huku akionyesha kuendelea kuwathamini wananchi wote na kuitikia ombi lao la kutoa pesa taslimu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa madarasa badala ya mabati 50 kama alivyoahidi hii ni kutokana na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa na desturi  ya kuhakikisha inapaua pindi wananchi wafikiapo hatua elekezi.

Akizungumza na wananchi Kwa niaba yake, Michael Kembaki  pamoja na chama cha mapinduzi katibu chama cha mapinduzi (CCM)  Hamisi Mkaruka Kura wakati akihutubia wazazi walezi pamoja na wananchi katika kikao cha kupanga mipango ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Nyamisangura ambapo ametoa  kiasi cha shilingi milioni moja laki mbili na elfu hamsini kama gharama za mabati hamsini yaliyohaidiwa  huku bati moja likihesabiwa kiasi cha shilingi  25,000/= ambayo ni kwa bei ya mabati imara.

Aidha Hamisi amewaasa wazazi kujitoa katika kuchangia michango kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo kwani kwa kufanya hivyo wataweza kupata mafanikio yatokanayo naelimu ambapo wataandaa mazingira mazuri ya maisha ya watoto wao pamoja na jamii kiujumla.

‘’Wazazi tutambue umuhimu wa elimu kwani baada ya watoto wetu kupata elimu watatusaidia sisi na familia zao,"alisema Mkaruka.

Pia Mkaruka ameeendelea kuhimiza wananchi kut kuwa na kigugumizi katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo pamoja na kuwa na desturi ya kuwa mstari wa  kwa kuanza kutekeleza miradi husika ili serikali pamoja na wadau mbali mbali waendelee kuwasaidia kufikia malengo husika na kuwahakikishia kuwa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania inayoongozwa na chama cha mapinduzi CCM chini ya kiongozi makini rais John pombe Magufuli ipo nao bega kwa bega katika jkutekeleza miradi mbalimbali katika kuhakikisha kuwa tunafikia uchumi wa viwanda.

Naye mmoja wa wazazi waliohudhuria kikao hicho,  Aakofu Fransisco  Stingo ametoa shukrani kwaniaba ya wazazi pamoja na wananchi amesema kuwa wamekuwa wakipiga kelele dhidi ya upatikanaji wa wadau wa maendeleo jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa vyumba vya madarasa vya kutosha  kwa haraka ambavyo vitamudu kuwastili wanafunzi wanaotarajia kujiunga na shule hiyo mwaka huu huku akiwaomba viongozi viongozi wa CCM kuwasaidia kutafuta wadau wa maendeleo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika maeneo mbalimbali jambo ambalo litasaidia ukamilifu wa vyumba hivyo kwa haraka.

Hata hivyo mwenyekiti wa UVCCM Wilayani Tarime, Godfrey Fransis ameweza kutoa wito kwa wanachi pamoja na kuwa na tabia ya kuwekeza katika elimu ambapo wataweza kupiga katika maendeleo kwani kwa kuzingatia hilo wataweza kufanikiwa katika maisha yao binafsi na maendeleo ya nchi kiujumla

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyamisangura , Steven Alexander Cheche pamoja na afsa elimu kata nyamisangura madam Vestina Maduso wamesema kuwa mapaka sasa wameweza kuanzisha ujenzi wa boma la ofisi ngazi ya lenta na majengo yanayofungwa linta madarasa matatu na ofisi moja na maandalizi ya misingi ya madarasa mawili na ofisi moja yanaendelea ambapo amedai kuwa ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi walioko majumbani wanahitaji madarasa sita ambapo wawanafunzi watasoma katika mazingura mazuri na rafiki.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia