Natamani kusikia Sugu na mchumba wake wameachana - Faiza Ally


Msanii wa Filamu Bongo, Faiza Ally ameeleza hisia zake baada ya baba mtoto wake, Sugu kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake.

Faiza amesema kiukweli anatamani asikie Sugu na mpenzi wake huyo wameachana na ndoa imevunjika vipande vipande.

"Mimi sina sababu ya wao kuwatakia heri, mimi sina sababu ya wao kuwaonyesha mapenzi yani i have no good reason kuwatakiwa kila kheri , kiukweli mimi siwatakii heri natamani kusikia wameachana, ndoa imevunjika vunjika kama kokote," amesema Faiza.

"Zaidi sana simpendi sana mwanamke kwasababu mwanzoni hata kama tumeachana alikuwa anamwangalia mtoto,  Lakini sisi wanawake tuna ile usimpigie mtoto atawapatanisha," Faiza ameiambia Wasafi Tv.

Wiki kadhaa zilizopita Sugu alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake, Happyness Msonga.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia