Ashley Cole kuungana na Frank Lampard Derby County

Klabu ya Derby County ya Uingereza ipo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili Ashley Cole kwenye dirisha hili la usajili ili aitumikie klabu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Cole mwenye miaka 38, kama akikamilisha usajili huo ataungana na Frank Lampard ambaye ndio kocha mkuu wa klabu hiyo.

Cole na Lampard walishawahi kucheza pamoja wakiwa Chelsea kwa mafanikio makubwa kabla ya kila mmoja kuondoka kwenye klabu hiyo kwa nyakati tofauti.