Beno Kakolanya ataka kuvunja mkataba Yanga SC


Golikipa wa Yanga SC, Beno Kakolanya kupitia mwanasheria wake ameandika barua kwa uongozi wa klabu hiyo akiomba kuvunja mkataba.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Samuel Lukumay amethibitisha kupokea barua kutoka kwa mwanasheria wa Beno hapo jana mbele ya waandishi wa habari.

“Mara ya kwanza tulipokea barua ya mwanasheria ikitaka Beno alipwe stahiki zake zote na Klabu ikafanya hivyo. Baada ya kumlipa Beno tulitegemea angeanza kuja mazoezini kuungana na timu kwajili ya kujiandaa na michezo inayotukabili lakini Beno hakufanya hivyo na bila taarifa," amesema.

Ameendelea kwa kusema, 'Hadi sasa Beno haidai Yanga ila Yanga inanamdai kwasababu mkataba wake unaisha 2020 lakini bado yeye ameendelea kushinikiza kuvunja mkataba,'.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia