.

1/14/2019

Diamond amtambulisha Tanasha kwa Mama yake


Hatimaye msanii Diamond Platnumz amemtambulisha mpenzi wake mpya, Tanasha kwa mama yake mzazi, Sanura Kassim Sandra.

Mahusiano na Diamond na Tanasha yalianza kugonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwaka jana na hata kuvishwa tetesi za ndoa. Hata hivyo wengi hawakutilia maanani iwapo muimbaji huyo atamtambulisha Bibie kwa familia yake.

Siku ya jana Diamond maarufu kama Simba akaonyesha ni kweli kakolea kwenye penzi la Bibie Tanasha pale alipomtambulisha kwa familia yake.

Katika video ambazo Diamond amezichapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram zimeonyesha Tanasha akisalimiliana na Bi. Sandra pamoja na Dada wa Diamond, Esma Platnumz.

Tanasha ambaye ni mrembo kutokea nchini Kenya anazidi kuwa maarufu Afrika Mashariki kwa kuwa mapenzini na Diamond. Awali Bibie alijizolea umaarufu nchini mara baada ya kuonekana kwenye video ya Alikiba na Christian Bella.