Diamond apiga marufuku wasanii kutoa rushwa Wasafi Tv/ Redio


Msanii wa Muziki ambaye pia ni C.E.O wa Wasafi Tv/ Redio Diamond Platnumz amepiga marufuku kwa wasanii kutoa hela ili yimbo zipigwe Wasafi Tv.

Diamond amesema hilo kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda na wasanii mbalimbali nchini.

"Pia naomba niseme hapa, Nimesikia kuna wasanii wanatoa fedha ili nyimbo zao zipigwe Wasafi Tv, pale hakuna kutoa hela, unavyotoa hela unataka nyimbo za wengine zisipigwe? kama kazi yako ni nzuri itapigwa tu na ukiendelea kutoa hela tutafungia kazi zako," amesema Diamond.

Msanii huyo amesema kuwa lengo la kuanzisha Wasafi Tv/Redio ni kuwasaidia wasanii wote na hivyo hataki kusikia habari ya msanii kutoa rushwa ili nyimbo zake zipigwe.
Mpya zaidi Nzee zaidi