Spika Ndugai ampa za uso Zitto ''Anapenda sana uongo"


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa habari ya Mbunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa amekalia ripoti ya ukaguzi wa CAG  si za kweli.

Spika Ndugai amesema kuwa Zitto anapenda sana tabia za uongo ambapo Mbunge huyo alitumia kurasa zake za kijamii kueleza hayo huku akisema kuwa haipendezi kuwa na tabia za uongo.

"Kwa mfano, aliandika katika mtandao wake kuwa nilipokea ripoti ya CAG tangu Januari 8, 2019 nikaikalia wakati mimi nimepokea taarifa hiyo Januari 16, 2019 na Januari 18, 2019 niliwapa kamati ya PAC. Ni vyema Watanzania wakajua huyu mwenzetu ni muongo," amesema Ndugai bungeni leo Alhamisi Januari 31, 2019.

Aidha Spika Ndugai amesema licha ya uongo huo ni mapema mno kumpeleka kiongozi huyo wa ACT katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Spika amesema kuwa kauli  zinazodai amekalia ripoti ya ukaguzi ya CAG  ya tril 1.5/- si za kweli na ni taarifa za Uongo zenye lengo za kumpaka Matope na hata Kamati ya PAC ilipoiuliza Ofisi ya CAG kuhusu ubadhirifu huo walisema hakuna ripoti kama hiyo.


Mpya zaidi Nzee zaidi