Diamond na Sallam wanashindana kuoa - Babu Tale


Meneje wa Msanii, Diamond Platnumz, Babu Tale amesema kuwa mwaka huu ni mwaka mkubwa kwa lebo ya WCB.

Tale amesema kuwa Sallam anapambana kuoa mke mwingine hivyo anashindana kuoa na msanii wake Diamond ambaye ametangaza ndoa ndani ya mwaka huu.

"Sallam anapambana kuoa mwanamke mwingine ilikuwa ni Februari naye anapambana na msanii wake Diamond kuoa tuwaombee tu dua ndio maana nasema mwaka huu ni mwaka mkubwa sana kwa WCB Wasafi tuwaombee dua," alisema Babu Tale Dizzim Online.

Babu Tale aliongeza kuwa "Sallam ameoa mke wa kwanza ambaye ni mzungu na wa pili aliyezaa nae hawajabahatika kuoana ila mwaka huu anaongeza mke mwingine.