Baada ya vuta ni nikuvute iliyotokea hivi karibuni, Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeeleza kuwa lina mahusiano mazuri na wasanii wa WCB.
Akizungumza na Wasafi TV ofisini kwake, Katibu wa Basata, Godfrey Mngereza amesema kuwa wanaendelea vizuri na wasanii wa WCB kuna baadhi ya nyimbo wamepeleka mashairi yake yakaguliwa kabla ya kutoka.
"Kuna kazi baadhi ambazo wamezileta ambazo baadhi Baraza wanazipitia na wataendelea kuwepo na tuna mahusiano mazuri sana," amesema.
Utakumbuka hivi karibuni Basata waliufungia wimbo wa Rayvanny na Diamond uitwao Mwanza kutokana na kukiuka maadili, pia wimbo huo ulipelekea hadi wasanii hao kufungiwa muziki ingawa adhabu yake ishatenguliwa.
