Kesi ya Zitto; Mahakama Kuu yamuita Spika sakata la CAG


Mahakama Kuu imetoa wito kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kufika mahakamani leo kwenye kesi ya kikatiba kuhusu kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kesi hiyo itakapotajwa kwa mara ya kwanza.

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 01/2019 imefunguliwa Mahakama Kuu, Masjala Kuu na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe dhidi ya Spika.

Zitto Kabwe ameiomba mahakama itoe tafsiri ya kinga ya CAG iliyopo kikatiba na tafsiri ya sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge katika kushtaki wanaodaiwa kulidhalilisha Bunge.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items