.

1/06/2019

Fahamu saikolojia ya mahusiano ya kimapenzi ilivyoMwanaume hupenda kuanzia asilimia 100 na kisha kuanza kushuka chini. Mwanamke  hupenda kuanzia asilimia 0 na kisha huanza kupanda hadi 100 na ndio maana mwanaume ambaye humfuata mwanamke na kumtongoza yaani kumshawishi apende, mwanamke akishaanza kupenda huanzia 0 na kuendelea kuongeza upendo.

Wakati huu mwanaume humsikiliza mwanamke kwa kila kitu, na huonekana kama bwege wala sio bwege bali yupo katika asilimia mia za mapenzi, mwanamke hukutana na mwanaume katika asilimia 50 za mapenzi yaani yeye anapanda na mwanaume anashuka hapa mapenzi huwa motomoto kwa pande zote mbili, yaani hakuna anayetaka kubabaishwa kila mtu anajua kuliko mwenzake

Cha kustaajabisha hapa hata mkiachana hakuna anayelia kuwa ametendwa, Lakini baada ya hapo mwanaume hushusha upendo chini ya asilimia 50. Wakati wa mwanamke unazidi kupanda juu zaidi ya 50. Mwanamke anapofikisha asilimia 100 wakati mwanaume akiwa na asilimia chini ya 40 ni hapa mwanamke huanza kuhisi
anaibiwa mara kwa mara na mwanaume naye huisi kuwa mwanamke yule ameisha
ladha.

Katika hali hii wakiachana utamsikia mwanamke anasema ‘NIMETENDWA’. Lakini
hajatendwa sema alikuwa anapenda mtu ambaye alikuwa anapenda zamani. Ukimsikia mwanaume anasemakuwa ametendwa basi ujue huyu alikuwa katika asilimia 80 wakati
ndo kwanza msichana yupo katika 10%.

ANGALIZO.
Penzi la mwanaume huja haraka kama kasi ya 4g na huondoka upesi vilevile. Penzi la mwanamke ni gumu kulipandisha kama ilivyo kumfikisha kileleni na ni hudumu muda mrefu kama ambavyo mwanamke aliyefika kileleni anavyodumu katika raha muda mrefu.