1/11/2019

Hakuna nchi iliyoendelea kwa kupewa misaada - Rais MagufuliRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hakuna nchi iliyoendelea kwa kupewa misaada.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 11, 2019 katika hafla ya kupokea ndege ya pili  aina ya Airbus A 220-300 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

"Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa hakuna nchi iliyoendelea kwa kupewa misaada, haipo nchi duniani iliyotoka kwenye umaskini ikafanikiwa ikawa tajiri kwasababu ilipewa misaada na nchi nyingine itafuteni hamta ipata," alisema Rais Magufuli.

Utakumbuka serikali katika jitihada za kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hadi sasa serikali imenunua ndege aina ya Bombardier Q400 tatu, pamoja na Boeing 787-8 Dreamliner na Airbus 220-300, na leo imewasili nyingine aina ya Airbus 220-300.