Kauli ya kwanza ya Alikiba baada ya kifo cha Baba yake mzazi


Mapema alfajiri siku ya jana Baba wa msanii wa msanii wa Bongo Fleva, AliKiba alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Kwa mara ya kwanza tangu muimbaji huyo kufiwa, amechapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii kuelezea kifo cha baba yake.

"Nawashukuru wote walioshiriki katika mazishi ya mzee wangu Na wale ambao hawakujaaliwa pia mimi Na familia yangu tumefarijika sana namuomba MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali Pema peponi Na atupe subira kwenye kipindi hiki kigumu AMIN," ameeleza Alikiba. 

Kabla ya kufariki Mzee Saleh Kiba alikuwa akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili toka December 27 mwaka jana hadi umauti ulipomfika, alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.