1/11/2019

Kayumba afunguka kutoka kimapenzi na Irene UwoyaMsanii wa Muziki Bongo,  Kayumba ameongea kuhusu kutoka Kimapenzi na msanii wa Filamu,  Irene Uwoya.

Kayumba amesema kuwa watu wasipate tabu kuona yuko karibu na msanii, ila kama wanadhani yuko na Uwoya basi waendelee kufikiria hivyo.

"Irene Uwoya ni msanii mkubwa sana Tanzania na ijulikane hivyo, unapokuwa na ukaribu naye lazima story kama hizo ziwepo naweza kusema siwezi kuwazuia watu kuongea, lakini mimi ndiye ninayejua ukweli na yeye ndiye anayejua ukweli uko wapi," alisema Kayumba EATV.

 Irene Uwoya ilidaiwa alifunga ndoa na Dogo Janja ambapo mpaka sasa inadaiwa kuwa wameachana hali ambayo hakuna hata mmoja kati yao aliyedhibitisha hilo.