Kichuya sasa rasmi ENPPI

Klabu ya Simba imesema kuwa uhamisho wa kiungo wake Shiza Kichuya umekamilika na kuanzia kesho ataanza mazoezi na timu yake mpya ya ENPPI kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Al Ahly utakaochezwa siku ya Jumanne Februari 5, 2019.

Kichuya ambaye ametamba na klabu ya Simba anatarajiwa kuanza maisha mapya ya soka nchini Misri kwenye klabu yake mpya.
Mpya zaidi Nzee zaidi