Mchungaji mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji amewaombea wasanii wote nchini viwanja na sehemu ya kulala.
Masanja ametoa ombi hilo kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda na wasanii mbalimbali nchini.
"Mkuu wa Mkoa tunaomba utusaidie pa kulala tulale sehemu kwa amani, Mkuu wa Mkoa tusaidie bwana si kuna maviwanja huko mnapima tupe priority kama wasanii au nakosea? Alihoji Msanja.
"Nawabembelezea mnasumbuliwa kwenye nyumba za kupanga, mimi nimeshajenga nawasaidia alafu mnazubaa basi freshi basi freshi Mh. Paul," aliongeza Masanja.
Masanja aliendelea kusema kuwa hakuna kuongelea nyuma ya camera kwasababu hata wenye camera (Waandishi wa habari) wanasumbuliwa vile vile kwasababu nao wanakaa kwenye nyumba za kupanga na wanasumbuliwa vile vile.