Na. Rahel Nyabali, Tabora.
Wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Tabora wasichana iliyopo Manispaa ya Tabora wameiomba Serikali na wadau wengine wa masuala ya elimu kuwajengea uzio katika shule hiyo kwani wamekua wakipata adha kubwa kutokana na watu kuingia shuleni hapo mara kwa mara kutokana na eneo la shule hiyo kuwa wazi kwa kukosa uzio .
Wakizungumza na Muungwana Blog baadhi ya wanafunzi hao, wanasema wamekua wakipata usumbufu mkubwa hasa nyakati za usiku, kutokana na watu kuingia na kutoka shuleni hapo bila ya kuwa na shughuli maalumu jambo ambalo wanadai linahatarisha usalama wao.
Happyness Boaz ambaye ni mwanafunzi Tabora girls amesema mara nyingi wamekua wakiibiwa vitu mbalimbali katika eneo la shule jambo linalo sababisha kuishi kwa wasisiwasi ilhali ni shule ya wasichana jambo ambalo linasababisha kusoma kwa wasiwasi wakati wa usiku.
"Tunatatizo kubwa ukizindhatatia hii ni shule ya wasichana inatulazimu tusome kwa mda mfupi wakati wausiku kwa sababu tunakosa amani na mtu mwenye nia mbaya anaweza akaja akafanya chochote hata tukianika nguo tunaibiwa hapa watu wanapita kama njia kwa sababu hakuna uzio.’’ Amesema happiness.
Kutokana na changamoto hiyo inayo wakumba wanafunzi katika shule hiyo kongwe ambayo kwa sasa ina wanafunzi wapatao 800 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita shule inayomilikiwa na Serikali.
Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini, Emmanuel Mwakasaka amenyeshwa kuguswa na hali hiyo na kukabidhi kiasi cha saruji shuleni hapo ili kufanikisha ujenzi wa uzio katika shule hiyo ikiwakilishwa na Katibu wa Mbunge huyo Lucas Masanja .
Mkuu wa shule hiyo Lydia Mwampamba ameshukuru msaada huo wa seruji na kuwaomba wadau kusaidia ujenzi wa uzio katika shule hasa katika mabweni ili kuongeza ulinzi katika eneo la shule hiyo jambo ambalo litasaidia kuongeza ufaulu katika shure hiyo.
