Kitu pekee kitakachokupa hamasa ya mafanbikio ni hiki

Asante kwa kuendelea kutembelea mtandao huu kila wakati kwani ni imani yetu elimu zinazotolewa hapa zinakusudia kwa namna moja ama nyingine. Na siku ya leo nataka tuangazie macho na akili zetu katika kujiuliza swali lifuatalo;

Ni kitu gani kinachokupa hamasa katika kuteda mambo yako?

Watu wengi maisha yetu yamekuwa kila siku katika hali ya kawaida kwasababu tumekuwa hatujui ni kipi ambacho kimekuwa kikitusukuma katika kufikia malengo yetu.

Na katika hili kuna aina mbili ya hamasa ambazo zimekuwa zikimsukuma mtu katika kutenda au kutokutenda jambo hilo. Aina ya kwanza ambazo zimekuwa zimkimsukuma mtu kutenda jambo fulani ni hamasa ya hofu.

Hamasa hii ya hofu mara nyingi mtu hufanya jambo fulani si kwa kupenda kutoka nafsini mwake, bali ni kwa kumgopa mtu fulani.

Kwa mfano hivi hujawahi kuona mtu anawahi ofisini eti kwa sababu anamgopa bosi wake? Bila shaka umewahi kuona aina hii ya watu. Tuendelee kutafakari kidogo hivi hujawahi kuona mtu anaendesha chombo cha usafiri nyakati za usiku sana eti kwa sababu anawakwepa askari wa usalama barabarani? Bila shaka umewahi kuona aina hii ya watu.

Aina hizi za tabia ndizo tunazozita hamasa za hofu, unafanya jambo kwa sababu ya kumuogopa mtu fulani,lakini ukweli ni kwamba  aina hii ya hamasa si nzuri kuitumia kama kweli unataka mafanikio ya kweli.

Ila kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli kila wakati unahitaji "hamasa ya upendo" katika kutenda mambo yako ya kimafanikio. Mara nyingi unashauriwa kufanya kitu kwa kukipenda kitu hicho kutoka nafsini mwako. Kwa mfano kama unafanya kazi usifanye kazi kwa sababu unamuogopa bosi wako bali fanya kutokana upendo ulionao juu kazi yako.

Usifanye kitu kwa kuwaridhisha watu wengine bali ifanye kazi yako kutokana na dhamira amabayo inakusukuma kutoka nafsini mwako. Ukifanya kitu kutoka nafsini mwako itakufanya ufanye kazi kwa moyo wako wote kwani utafanya kazi ambayo utakuwa unaipenda, na italeta matokeo chanya.

Hivyo kila wakati afisa mipango nasisitiza ya kwamba kwa kila kitu ambacho unakifanya hakikisha unakifanya kitu hicho kwa sababu ya upendo wa dhati juu ya kitu hicho, na sio kufanya jambo fulani kutokana na hofu.

Pia hakikisha ya kwamba hofu hauipi kipaumbele katika maisha yako kwani hofu ni chukizo mbele ya Mugu na mafanikio yako kwa ujumla.

Kabla sijamaliza nikukumbushe tu ya kwamba maisha ni kuchagua, hivyo jiulize sasa kipi ambacho  kitaongoza maisha yako je hofu au upendo? Usinipe jibu.

Na. Benson Chonya.