.

1/06/2019

Kocha wa Fenerbahce apendekeza Samatta asajiliwe haraka katika Timu yake


Kocha wa Fenerbahce, Ersun Yanal amependekeza Mbwana Samatta asajiliwe haraka kwenye Kikosi hicho.

Habari zinasema kwamba, mabao pamoja na asisti za Samatta hasa kwenye Europa ndizo zimemchanganya kocha huyo na akaulazimisha uongozi utoe fungu haraka umsajili.

Kocha huyo amefikia uamuzi huo kutokana na mastaa alionao akiwemo Andrew Ayew wa Ghana kushindwa kung’ara kama Samatta ambaye kwa sasa ana mabao 15 kwenye Ligi ya Ubelgiji akiwa na Klabu yake ya Genk.

Mbali na Samatta ambaye sasa nyota yake inang’ara kila kona, pia kocha huyo yuko kwenye mpango wa kuwanasa Marouane Fellaini wa Man United na Cesc Fabregas wa Chelsea.

Fenerbahce imepanga kutumia dirisha dogo la usajili kupangua kikosi hicho ambacho kimekuwa kikifanya vibaya kiasi cha kushika nafasi ya pili kutoka mkiani mwa ligi yenye timu 18. Timu hiyo imeshinda mechi tatu kati ya 17 ilizocheza mpaka sasa.