Kocha wa Yanga SC kumleta kiungo mpya


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amesema kuwa kumfanya kiungo wake, Feisal Salum ‘Fei Toto’ awe na uwezo wa hali ya juu, atamletea kiungo mpya ambaye atampa changamoto ya kugombania namba.

Fei Toto ambaye alitua Yanga msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar, kwa kiasi kikubwa amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji ndani ya kikosi hicho cha Yanga. Viungo wengine ambao wanacheza sambamba na Fei ni pamoja na Papy Tshishimbi, Raphael Daud na Maka Edward.

Zahera amesema kwamba anatarajia kumpa ushindani Fei kwa kumleta kiungo Gustapha Simon kwenye timu ya wakubwa ili kutoa changamoto ya namba kwa wachezaji waliokuwepo.

“Yule mtoto (Gustapha) anajua sana na naamini akija huku timu ya wakubwa basi ataleta changamoto ya hali ya juu sana. Hawa kina Fei Toto na Tshishimbi watakuwa na kazi kubwa sana ya kugombania naye namba.

Hata hivyo amesema alimuona alichofanya katika Kombe la Mapinduzi  ana uwezo wa hali ya juu katika kuendesha timu lakini pia kuichezesha timu, akienda timu ya wakubwa asi atafanya vizuri.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items