Wanafunzi waliofaulu 2059 kukosa masomo


Na Timothy Itembe Mara,

MBUNGE wa jimbo la Tarime Vijijini,John Heche kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema amechangia Mabati 577 katika halmashauri ya Tarime Vijijini kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kujenga vyumva vya madarasa na kuhakikisha kuwa wanafunzi waliofaulu mwaka jana na kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza wanapata vyumba vya kusomea.

Akiongea jana katika kikao cha baraza la madiwani Kaimu Mkurugenzi ambaye ni Afisa Mifugo na Uvuvi,Peter Nyanja alisema kuwa katika jitihada za kuhakikisha kuwa wanafunzi waliofaulu mwaka jana na kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanaanza masomo mwezi Februali mwaka huu na katika juhudi hizo Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Johnh Heche amechangia mabati 577 kupitia fedha ya mfuko wa jimbo.

Nyanja aliongeza kuwa kwa mwaka 2018 wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba ni watoto 5367 kati yao waliochaguliwa kwenda shule za Bweni ni wanafunzi 15 huku waliochaguliwa kwenda shule mbalimbali za sekondari yaani kutwa ni 3293 na  wanafunzi 2059 walikosa nafasi ya kuchaguliwa ili kujiunga na sekondari kutokana na upungufu uliopo wa vyumba vya madarasa 47.

Pia Nyanja aliongeza kuwa katika halmashauri yake wametenga fedha kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo ili kuhakikisha kuwa ifikapo Februali 2019 wanafunzo wote waliofaulu mtihani wanaingia sekondari na kuanza masomo,Nyanja alitaja shule za sekondari katika halmashauri yake kuwa zipo shule za sekondari za serikali 30 huku shule za binafsi zikiwa 3.

Wakati wakijadili madiwani katika Baraza hilo Mmoja wa madiwani hao,John Bosco wa kata ya Regicheri kupitia chama Cha Mapinduzi (CCM) alihoji kutaka kujua ni lini halmashauri hiyo itakamilisha vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari ili wanafunzi walikoswa nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wapange mashuleni ili kuanza masomo.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items