Lema apingana na Spika kuhusu matibabu ya Lissu, asema atajiuzulu


Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema amesema ajitihuzulu kwenye nafasi hiyo iwapo Spika wa Bunge, Job Ndugai atathibitisha ni kweli bunge limechangia matibabu ya Tindu Lissu.

Godbless Lema ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter baada ya Spika kueleza kuwa Lissu kapatiwa Tsh. Milioni 250 za matibabu.

“Bunge halijawahi kumlipia Lissu pesa kwa ajili ya matibabu, alichokisema Mh Spika Ndugai ni
upotoshaji kwa jamii na Mungu.Chama kitatoa tamko juu ya hili.Spika akiweza kuthibitisha hili,Mimi nitajiuzulu Ubunge,mshahara wa Mbunge sio hisani ya Spika," ameeleza Lema.

Mapema leo asubuhi Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amesema  kauli zinazodai kuwa Ofisi ya Bunge haijawahi kumjali kifedha   Mhe. Tundu Lissu  tangu alipopata matatizo si za kweli kwani hadi kufikia mwezi Desemba 2018 ameshalipwa na Ofisi ya Bunge kiasi cha Tsh. milioni 250.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha