Maandamano yasababisha vifo vya watu wawili

Katika maandamano yanayoendelea nchini Sudan kwa muda unakaribi mwezi mmoja, watu wawili wameripotiwa kuuawa na wengine wanane kujeruhiwa mjini Khartoum.

Taarifa iliotolewa na kituo kimaoja cha matibabu  mjini Khartoum zimefahamisha kwamba  watu watatu wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi za plastiki  huku wakingine wawili  wakifahamishwa kufariki katika maandamano kabla ya kufikishwa hospitali kupatiwa matibabu.

Raia wa Sudan walianza maandamano kuishinikiza serikali kupunguza bei za bidhaa uhimu ambazo ni mahitaji ya kila siku  nchini Sudan.

Maandamano hayo yalianza Disemba 19 Port-Sudan na Atbera.

Amir Muhammed Ä°brahim, muendesha mashataka mjini Khartoum katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi alitangaza kuwa watu 23 ndio waliokwishafariki  na wengine 131 wamejeruhiwa kutokana na maadamano yanayoendelea nchini Sudan huku upinzani  ukipinga idaidi hiyo kwa kusema watu walioua na waliojeruhiwa inazidi idadi iliotolewa na utawala.