Manchester United yapata pigo

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, amethibitisha kuwa mchezaji wake Marouane Fellaini atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu au nne baada ya kuumia mazoezini.

Solskjaer pia amemzungumzia Scott McTominay kuwa ataendelea kusalia Old Trafford kwa kipindi hiki kilichobaki cha msimu huu, kwahiyo hatotolewa kwa mkopo kutokana na Fellaini kuwa majeruhi.

Aidha Solskjaer amesema, Fellaini ataendelea kujituma ili kurudi kwenye mechi kubwa zijazo.