Mhandisi aswekwa ndani kwa amri ya Waziri


Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ameliagiza jeshi la polisi mkoani Shinyanga kumkamata mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba kwa kushindwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa maji.

Ametoa agizo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo kwenye mkutano wa hadhara ambapo wananchi waliopewa nafasi ya kuuliza maswali walijikita na changamoto ya upatikanaji wa maji kutokana na mradi uliopo kushindwa kutoa maji.

“Mradi wa maji Mwakitolyo gharama yake ni shilingi bilioni 1.482 mpaka sasa serikali ya imelipa kiasi cha bilioni 1.462, sisi tunaumia sana wakati mwingine huyu angekuwa daktari si angeshaua watu, mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ita polisi peleka ndani mtu huyu” ,alisema Aweso.

Hatu hiyo ilifiki baada ya majibu ya mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba yalishindwa kujitosheleza licha ya serikali kutoa fedha kiasi cha Tsh. Bil. 1.4.