Simba wajipanga kuujaza Uwanja katika mechi yao dhidi ya Waarabu


Ofisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Manara, amesema wamejipanga kuujaza Uwanja Kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya SJ Saoura ya Algeria Januari 12 mwaka huu.

Ofisa huyo ameeleza kuwa tayari wameshaanza kampeni maalum ya kuhakikisha Uwanja wa Taifa unajaa vilivyo.

Manara amesema anaamini Simba itafanya vema katika kipute hicho kinachosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka hapa nchini.

Simba itakuwa inakutana na Saoura baada ya kufanikiwa kuwaondoka mashindanoni Nkana Red Devils kwenye hatua ya kwanza ya mashindano.