.

1/14/2019

Ujumbe wa RC Makonda kwa Hamisa Mobetto, 'Hili lisikupe tabu'


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameteka ghafla mazungumzo mtandaoni kufuatia ujumbe uliomwandika Mwanamitondo Hamisa Mobetto.

RC Makonda ametumia ukurasa wake wa Intagram kuweka video ya Hamisa Mobetto na kuisindikizia na ujumbe uliosomeka;'Mama kwa uzoefu nilionao hili lisikupe tabu'.

Ujumbe huo ulikuja zikiwa ni saa chache kupita tangu kwa muimbaji Diamond Platnumz kumtambulisha mpenzi wake Tanasha kwenye familia yake.

Utakumbuka Diamond na Hamisa Mobetto wamejaliwa kupata mtoto mmoja katika mahusiano yao ambayo waliyafanya siri kwa kipindi kirefu. Tetesi ziliwahi kudokeza huenda wawili wangekuja kufunga ndoa, hata hivyo hilo linaoneka kuota mbawa kwa sasa.